Badilisha Maisha – Jifikiriye Binafsi!

Badilisha Maisha – Jifikiriye na Kuwa Binafsi Badala Yake!

Translated from English – Be Selfish For A Change! Swahili!

December 15, 2018!

Kama miaka mingi iliopita nilipofanyiwa Operation Royal Hospital hapa Muscat Oman – sijuwi kwa ajili ya Operation au kwa ajili ya huzuni na matokeo baada ya operation – nilikuwa juu ya kitanda nalia sana kwa kikukuwi!

Huyu Daktari N wa KiOmani wa Kikee akaniuuliza – Baba unaliya kwa ajili ya nini? Wewe ni mtu mzima na haifai kulia hivi – unafanya uchura haifai! Nini kimetokeya? Na khasa jana tu umefanyiwa operation kubwa nah ii kulia itakuleteya aathiir na matokezi sio mazuri badala yake!

Nikamwambiya sasa ni saa 11.30 jioni (5,30 pm) na imebaki nusu saa tu watu kuruhusiwa kuingiya kutembeleya Wagonjwa – na mpaka sasa hajaja mtu kuja kunitizama!

Akanihujumu na kunishauri kwa sauti kali – Ni hilo tu? Na unaliya kwa ajili ya hayo? Kumbuka katika Maisha siku zote uwe na ufanye hivi – ikiwa watu watakuja au hata hawata kuja!

Wa Kwanza ni Majid – Wewe!
Wa Pili ni Majid – Wewe!
Wa Tatu ni Majid – Wewe!
Wa Nne ni Majid – Wewe!
Wa Tano Watoto wako Family yako Mke (na Wajukuu!)

Waliobaki katika Maisha yako waache wajipange mstari queue wenyewe – usiwapuuze lakini pia usiwa unawajaali sana kufikiya lengo la kujiuumiza nafsi yako!

Kumbuka haya siku zote!

Kuwa Binafsi badala yake! (Yaani piga moyo konde!)

Unaonesha kuwa ni mtu anayejaali watu wengi sana – na hata kujiuumiza na kujidhuru nafsi yako!
Hawa watu hawastaahili kufikiriwa hivi na wewe kuanzia sasa!

Samahani lakini pia! Mimi nimesha kuona kuwa ni mtu mzuri mkarimu na daima una wafikiriya watu – lakini Duniya sasa imebadilika sana – hamna Imaani Taqwa Ihsaani na Wema!

Samahani kwa Kiswahili – miaka mingi tangu kuandika kwa Kiswahili!

AL HAMDU LILLAH!!

From The Book – That Is The Way It Is! Between Us Only!
By Majid Al Suleimany – http://www.myownmajid.com